KLABU ya Liverpool imekubaliana na klabu ya Lille ya Ufaransa kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji ambaye ni mzaliwa wa Kenya Divock Origi. Klabu hiyo pia imepania kumsajili kiungo wa kati wa kimataifa wa Serbia na klabu ya Benfica Lazar Markovic. Liverpool imekubali kutoka kitita cha paundi milioni 10 kwa ajili ya Origi ambaye ana umri wa miaka 19 na mazungumzo kuhusiana na suala hilo yatarajiwa akukamilika baadae wiki hii wakati Markovic yeye anatarajiw akutengewa kitita cha paundi milioni 25. Mazungumzo ya kusajiliwa kwa nyota hao yanakuja huku ikifahamika kuwa Liverpool inatarajia kumuuza mshambuliaji wake nyota Luis Suarez kwenda Barcelona kwa ada ya paundi milioni 75.
No comments:
Post a Comment