Friday, July 11, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: FIFA YAMKAZIA SUAREZ.

SHIRIKISHO la soka Duniani-FIFA limetupilia mbali rufani iliyokatwa na Shirikisho la Soka la Uruguay kupinga kufungiwa kwa mshambuliaji wake Luis Suarez kwa kosa la kumng’ata beki wa Italia katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Katika taarifa ya FIFA iliyotumwa katika vyombo vya habari imeeleza kutupilia mbali ombi hilo la kupunguza adhabu ingawa hata hivyo bado mchezaji huyo anaweza kukata tena rufani katika Mahakama ya Rufaa ya Michezo-CAS kama hataridhika na uamuzi huo. Suarez mwenye umri wa miaka 27 alifungiwa na FIFA kutojishughulisha na mambo yoyote yahusuyo soka ka kipindi cha miezi minne sambamba na mechi tisa za kimataifa kwa tukio hilo. Tukio hilo lilikuwa la tatu kwa mshambulizi huyo bora msimu uliyopita katika Ligi Kuu nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment