Friday, July 11, 2014

SANCHEZ RASMI ARSENAL.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Chile, Alexis Sanchez amekamilisha usajili wake wa kuhamia klabu ya Arsenal akitokea Barcelona kwa mkataba wa muda mrefu uliogharimu kitita cha paundi milioni 35. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 amefunga mabao 47 katika mechi 141 alizoichezea Barcelona huku akifunga pia mabao mawili katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu. Akihojiwa Sanchez amesema amaefurahishwa kujiunga na klabu hiyo ambayo ina meneja bora, kikosi imara na mashabiki wengi kutoka kona mbalimbali duniani. Baada ya Sanchez Arsenal sasa inahamishia nguvu zake katika kumsajili beki wa kulia wa kimataifa wa Ufaransa Mathieu Debuchy mwenye umri wa miaka 28 kutoka klabu ya Newcastle United.

No comments:

Post a Comment