Wednesday, July 9, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: KLOSE ARUDISHA REKODI YA MABAO UJERUMANI.

MSHAMBULIAJI mkongwe wa kimataifa wa Ujerumani Miroslav Klose ameweka rekodi ya kuwa mfungaji mabao mengi zaidi katika historia ya michuano ya Kombe la Dunia. Klose alifunga bao la pili wakati Ujerumani ilipowadhalilisha wenyeji wa michuano hiyo Brazil kwa kuwafunga mabao 7-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa huko Belo Horizonte. Klose mwenye umri wa miaka 36 sasa amefikisha mabao 16 aliyofunga katika fainali nne za Kombe la Dunia alizocheza. Kabla ya kufikia rekodi hiyo Klose alikuwa amefungana na nyota wa zamani wa Brazil Ronaldo aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo kwa kufunga mabao 15. Rekodi ya awali ya mabao ilikuwa ikishikiliwa na mchezaji wa Ujerumani Gerd Mulluer.

No comments:

Post a Comment