Wednesday, July 9, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: BRAZIL YAOMBOLEZA KIPIGO CHA MABAO 7-1 KWA VURUGU.

WANANCHI wa Brazil wamekuwa wakilia kwa uchungu huku wakimlaani rais wao na kuziba nyuso zao kwa aibu baada ya timu yao ya taifa pendwa kupata kipigo cha fedheha cha mabao 7-1 kutoka Ujerumani kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia uliochezwa jana. Baada ya timu hiyo kufungwa bao la tano kabla ya muda wa mapumziko mamia ya mashabiki waliacha siti zao za gharama na kuondoka uwanjani huku wakiwa na majonzi makubwa. Baadhi ya mashabiki waliobakia uwanjani wlaikuwa wakiimba nyimbo za kuwatukana na kuwadhalilisha wachezaji na rais wan chi hiyo Dilma Rousseff, ambaye kabla ya kuanza kwa alikumbana na upinzani kutoka kwa waandamanaji ambao walikuwa wakipinga gharama kuwa ya zaidi ya dola bilioni 11 kuandaa michuano hiyo. 
Mabomu ya machozi yalianza mapema kabla ya filimbi ya mwisho kutokana na bao la tatu la Ujerumani lililosababisha watoto na watu wazima kuanza kuondoka uwanjani na wengine kuacha luninga za jumuiya na kuingia mitaani hivyo polisi kulazimika kuimarisha ulinzi. Wakati mabao yalivyokuwa yakizidi kuingia zaidi ndivyo mashabiki walivyozidi kupandwa na hasira huku wengine wakishindwa kuvumilia na kumwaga machozi hadharani. Kipigo hicho pia kinaonekana kuwa na athari kuwa siasa za nchi hiyo hususani katika uchaguzi mkuu wa rais Octoba mwaka huu ambapo kuna hati hati ya Dilma kushindwa kutetea kiti chake kutokana na matokeo hayo.

No comments:

Post a Comment