Wednesday, July 9, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: NITUPIENI LAWAMA ZOTE MIMI - SCOLARI.

KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Luiz Felipe Scolari amekielezea kipigo cha mabao 7-1 walichopata katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani kuwa siku mbaya katika maisha yake na kudai kuwa lawama zote anapaswa kutupiwa yeye. Katika mchezo huo wenyeji walikuwa nyuma kwa mabao 5-0 kufikiwa muda wa mapumziko na kupelekea Ujerumani kutinga hatua ya fainali kwa staili ya aina yake. Scolari amesema anajua atakumbukwa kama kocha aliyefungwa mabao 7-1 lakini alijua hatari hiyo wakati akichukua kibarua cha kuinoa nchi hiyo ndio anataka lawama zote apewe yeye kutokana na mbinu na kikosi alichochagua. Scolari aliwaomba radhi wananchi wote wa Brazil kwa kipigo hicho cha kufedhehesha na kushindwa kufika fainali huku akidai watajaribu walau kushinda mecgi yao ya kutafuta mshindi wa tatu itakayochezwa Jumamosi hii.

No comments:

Post a Comment