KLABU Barcelona imedai kuwa mshambuliaji nyota wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez sasa amekuwa mchezaji wa timu hiyo kwa asilimia 100. Uhamisho wa mchezaji huyo uliowagharimu kiasi cha paundi milioni 75 ulikamilika wiki iliyopita lakini Barcelona walishindwa kumtangaza Suarez kwa mashabiki wao kutokana na adhabu ya miezi minne anayotumikia kwa kosa la kumng’ata beki wa Italia Giorgio Chiellini. Hata hivyo, mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Andoni Zubizarreta alithibitisha taarifa kwa vyombo vya habari na kudai kuwa nyota huyo ameshakuwa mchezaji wao rasmi. Suarez hataruhusiwa kuichezea Barcelona au kufanya mazoezi na wachezaji wenzake mpaka Novemba mwaka huu labda rufani yake aliyokata katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo-CAS itakapofanikiwa.

No comments:
Post a Comment