Tuesday, August 12, 2014

ANCELOTTI AWASHUSHUA WANAOMTAKA KHEDIRA, ADAI HANA MPANGO WA KUMUUZA.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amevionya vilabu vya Arsenal na Chelsea kumuacha Sami Khedira kwani kiungo huyo hauzwi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani amekuwa akihusishwa kuondoka Santiago Bernabeu toka waliposhinda Kombe la Dunia mwezi jana huku Uingereza pakitajwa kama kama uelekeo wake. Usajili wa Mjerumani mwenzake Toni Kroos kutoka Bayern Munich ndio ulionekana kuchangia kwa kiasi kikubwa nyota huyo kuhusishwa na kuondoka lakini Ancelotti amekanusha tetesi hizo na kudai kuwa Khedira bado ana mkataba nao unaomalizika kiangazi mwakani hivyo bado atabakia klabu hapo kwa kipindi hiki. Madrid wanahatarisha kumkosa Khedira bila kupata chochote kama wakishindwa kumshawishi asaini mkataba mpya wa mabingwa hao wa Ulaya wakati wa msimu 2014-2015.

No comments:

Post a Comment