CHAMA cha Soka nchini Ghana-GFA kimeunda kamati ya watu watatu itakayokuwa na jukumu la kuteua mshauri wa ufundi katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo, Black Stars. Hata hivyo maofisa wa GFA wamesisitiza kuwa mshauri wa ufundi atakayeteuliwa atakuwa na jukumu la kusimamia mfumo mzima wa Stars na sio kocha pekee. Umuazi wa kuteua kamati hiyo kwa mujibu wa taarifa ya GFA umepelekwa katika kikao cha kamati ya utendaji ya chama hicho kufuatia kupitia muelekeo wa ufundi wa kikosi cha timu ya taifa. Kamati hiyo ya watu watatu itaongozwa na makamu wa rais wa GFA Fred Crentsil ambaye atafanya kazi sambamba na Fred Pappoe na Francis Oti Akenteng. Taarifa ya GFA iliendelea kudai kuwa kamati hiyo itafanya pamoja na kocha wa Black Stars Kwesi Appiah ili kutafuta mtu atakayeweza kuipeleka timu ya taifa katika muelekeo unaofaa.
No comments:
Post a Comment