Tuesday, August 12, 2014

CHAMA CHA SOKA ITALIA CHAPATA RAIS MPYA.

CHAMA cha Soka nchini Italia kimepata rais mpya Carlo Tavecchio aliyetangazwa jana. Tavecchio mwenye umri wa miaka 71 alikuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo toka mwaka 2009 lakini alithibitisha kugombea kugombea nafasi hiyo kufuatia uamuzi wa Giancarlo Abete kuamua kujiuzulu baada ya Italia kutolewa mapema katika michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Brazil Juni mwaka huu. Pamoja na kampeni zilizojaa utata huku akituhumiwa kwa masuala mbalimbali Tavecchio alipambana na kuhakikisha anamshinda mpinzani wake ambaye ni nyota wa zamani wa AC Milan Demetrio Albetini na kuteuliwa kuwa rais mpya wa FIGC. Kibarua cha kwanza cha Tavecchio kitakuwa ni kusaidia kutafutwa kwa kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo huku kocha wa zamani wa Juventus Antonio Conte akipewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment