Tuesday, August 12, 2014

CABALLERO ATAMBA KUCHUKUA NAMBA YA JOE HART, CITY.

GOLIKIPA mpya Willy Caballero ana hamu kubwa ya kuchukua nafasi ya Joe Hart kama golikipa namba moja wa Manchester City msimu huu. Kipa huyo wa kimataifa wa Argentina alisajiliwa akitokea Malaga Julai ambapo alicheza katika mechi yake ya kwanza ya kimashindano akiwa na mabingwa hao wa Ligi Kuu wakati walipotandikwa mabao 3-0 na Arsenal katika mchezo wa Ngao ya Jamii. Caballero amesema anatamani kuendelea kubakia katika nafasi hiyo wakati kikosi cha City kinachonolewa na Manuel Pellegrini kitakapoanza kutetea taji lake katika mchezo dhidi ya Newcastle United Agosti 17 mwaka huu. Kipa huyo alikiri kuwa anataka kuwa namba moja wakati akihojiwa na atafanya mazoezi kwa bidii ili kuhakikisha anamshawishi kocha wake kumpa nafasi ya kuanza.

No comments:

Post a Comment