Monday, August 11, 2014

ARTETA NAHODHA MPYA ARSENAL.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa Mikel Arteta ndiye atachukua mikoba ya unahodha wa timu hiyo kufuata uamuzi wake wa kumuuza Thomas Vermaelen. Wenger ambaye kikosi chake kiliitandika Manchester City katika mchezo wa Ngao ya Jamii jana katika Uwanja wa Wembley alikuwa akitaka nahodha mpya baada ya kumruhusu Vermaelen kwenda Barcelona na sasa amemua kumkabidhi mikoba hiyo Arteta. Kwa kipindi kirefu kiangazi hiki mustakabali wa Arteta umekuwa haueleweki lakini kwa taarifa hizi inaonekana kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 ataendelea kubakia klabuni hapo msimu huu. Beki mahiri wa kimataifa wa Ujerumani Per Martesacker ameteuliwa kuwa nahodha msaidizi wa klabu hiyo. Arsenal walikubalia Vermaelen kwenda Barcelona kwa paundi milioni 15 baada ya Manchester United kukataa kubalishana na beki wao Chris Smalling.

No comments:

Post a Comment