MENEJA mpya wa klabu ya Manchester United amepiga hatua moja katika kuimarisha kikosi chake baada ya kufanya mazungumzo na wachezaji sita akiwemo beki wa kulia Rafael. Wachezaji hao Marouane Fellaini, Wilfried Zaha, Nani, Shinji Kagawa na chipukizi Willy Keane wote walifanya mazungumzo binafsi kwa nyakati tofauti na kocha huyo mara baada ya mazoezi ya timu hiyo katika Uwanja wa Carrington. Inafahamika kuwa kocha huyo Mholanzi aliwaambia Fellaini, Zaha, Nani na Keane kuwa klabu hiyo itasikiliza ofa yoyote itakayotolewa dhidi yao. Katika orodha hiyo Rafael ndio jina ambalo halikutegemewa naye anaweza kuondoka na kupelekea timu hiyo kutafuta mchezaji mwingine anayeweza kucheza nafasi hiyo. Kiungo Anderson na mshambuliaji Javier Hernandez tayari wanajua kuwa United inaweza kuwauza kama ikitokea ofa yoyote ambapo Southmpton, Inter Milan, Tottenham Hotspurs, Atletico Madrid na Juventus wote wameonyesha nia ya kumtaka Hernandez.
No comments:
Post a Comment