Monday, August 11, 2014

AFUNGIWA MIEZI MINNE KWA KUMSUKUMA MWAMUZI.

SHIRIKISHO la Soka nchini Iran, limemfungia kwa miezi mitatu mchezaji nyota wa kimataifa wa nchi hiyo Payan Sadeghian baada ya kumsukuma mwamuzi aliyemtoa nje katika mchezo wa ligi. Kiungo huyo wa klabu ya Perspolis hakufurahishwa na uamuzi wa mwamuzi Mohammad Reza Akbarian katika mchezo dhidi ya Foolad hatua ambayo ilipelekea kumkimbilia mwamuzi na kumsukuma. Akbarian baadaye alimuonyesha mchezaji huyo kadi nyekundu na mchezaji alitupa mkono wake wa kushoto kumtukana mwamuzi kabla ya kutoka nje ya uwanja. Vyombo vya habari nchini humo vimedai kuwa mbali na adhabu hiyo Sadeghian pia ametozwa faini huku mwenyewe akiomba radhi kutokana na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment