MICHUANO ya Kombe la Kagame inayoandaliwa na Baraza la Michezo la Afrika Mashariki na Kati-CECAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi baadae leo jijini Kigali, Rwanda. Jumla timu 14 zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo ambayo itafikia kilele chake Agosti 24 huku mechi 34 zilitarajiwa kuchezwa katika viwanja viwili vya Amahoro na Nyamirambo. Wawakilishi wa Tanzania Bara Azam FC watatupa karata yao ya kwanza dhidi ya wenyeji Rayon Sport katika mchezo wa ufunguzi wa kundi A, mchezo ambao utatanguliwa na ule wa wawakilishi wa Zanzibar KMKM watakaomenyana na Atlabara ya Sudan Kusini. Azam itarudi tena uwanjani, Agosti 10 kumenyana na jirani zao KMKM, kabla ya kucheza na Atlabara Agosti 12 na kukamilisha mechi za kundi lake, kwa kumenyana na Adamma ya Ethiopia Agosti 16. Azam imechukua nafasi ya Yanga SC iliyoenguliwa na CECAFA kwa kushindwa kuthibitisha kupeleka kikosi cha kwanza.
No comments:
Post a Comment