LIGI Kuu nchini Uingereza inatarajia kutambulisha sheria mpya za jinsi kushughulikia majeruhi ya kichwani toka kuanza kwa msimu wa 2014-2015. Mchezaji anayepata jeraha la kichwa sasa anatakiwa kutolewa uwanjani na daktari wa klabu lazima aamue kama mchezaji anaweza kuendelea na benchi la ufundi. Msimu uliopita Tottenham walishambuliwa kwa kumruhusu golikipa Hugo Lloris kuendelea kucheza baada ya kuzimia katika mchezo dhidi ya Evrton uliomalizika kwa sare ya bila kufungana. Baada ya Lloris kupatiwa matibabu na kuzinduka meneja wa wakati huo Andre Villas Boas alimrudisha uwanjani kumalizia mchezo huo hatua ambayo ililalamikiwa vikali na wataalamu wa magonjwa ya kichwa na ubongo kuwa inaweza kuhatarisha uhai wa mhusika. Baadhi ya wadau akiwemo kocha wa klabu ya Leicester City iliyopanda Ligi Kuu msimu huu wanaamini mabadiliko hayo yatakuwa msaada mkubwa kwa wachezaji.
No comments:
Post a Comment