Friday, August 8, 2014

LIGI YA MABINGWA AFRIKA YAFIKIA PATAMU WIKIENDI HII.

KLABU kongwe nchini Tunisia, CS Sfaxien inamatarajia makubwa ya kusonga mbele katika michuano ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika wakati watakapokuwa wageni wa timu ya Ahly Benghazi ya Libya katika mchezo wa mkondo wa pili wa kundi B utakaochezwa baadae leo. Kikosi cha timu hiyo kinachonolewa na kocha Philippe Troussier kitajitupa uwanjani huku kikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuifunga Ahly Benghazi kwa mabao 3-1 katika mchezo uliochezwa jijini Tunis Mei mwaka huu. Kwasasa Sfaxien wanashikilia nafasi ya pili katika kundi lao nyumba ya E.S Setif na ushindi wowote leo utakuwa umewavusha moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali. Mechi nyingine katika kundi B itakayochezwa kesho timu ya Setif kutoka Algeria watawakaribisha Esperance ya Tunisia wakati Jumapili kutakuwa na mechi za kundi A ambapo TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC itachuana na Al Hilal ya Sudan wakati Zamalek ya Misri wataikaribisha AS Vita nayo ya DRC.


No comments:

Post a Comment