Wednesday, August 13, 2014

CAF YAZISIMAMISHA NCHI TATU KUTUMIA VIWANJA VYAO VYA NYUMBANI KUTOKANA NA EBOLA.

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF, limesimamisha michezo yake katika nchi tatu za Afrika Magharibi kutokana na kuathiriwa na ugonjwa wa Ebola. Nchi za Guinea, Sierra Leone na Liberia hazitaruhusiwa kuandaa mechi za CAF mpaka itapotolewa taarifa zaidi na badala yake watacheza mechi zao za nyumbani katika viwanja huru. Katika taarifa yake iliyotolewa jana CAF imedai kuwa ratiba kwa michezo mingine wanayoaiandaa itaendelea kama ilivypangwa kasoro nchi hizo tatu ambazo ugonjwa wa Ebola umeripotiwa kuathiri watu wengi. Taarifa hiyo ilitaka Shirikisho la Soka kwa nchi husika kubadilisha ratiba kwa kutafuta viwanja huru kwa ajili ya mechi zao za nyumbani hususani katika kipindi cha Septemba mwaka huu. Ratiba itakayoathirika na mabadiliko hayo ni ya mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kundi E kati ya Guinea na Togo na mchezo wa kundi D kati ya Sierra Leone na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-RDC. Maofisa wa soka wa Sierra Leone tayari wameanza mipango ya kuhamishia mchezo wao huo jijini Accra, Ghana. Ugonjwa wa Ebola mpaka sasa umeashaua watu 373 nchini Guinea, 323 nchini Liberia na 315 nchini Sierra Leone na mpaka sasa haujapatiwa tiba sahihi wala kinga ingawa Liberia wameanza kutumia dawa za Zmapp ambazo hazijawahi kufanyiwa majaribio.

No comments:

Post a Comment