ILI kukuza soka la wanawake katika ukanda huu, Baraza la Michezo la Afrika Mashariki na Kati-CECAFA linajipanga kuandaa michuano ya kwanza ya wanawake mwaka 2015 ambapo wanatarajia kushirikisha nchi nane. Kwa mujibu wa makamu wa rais wa CECAFA Lawrence Mulindwa, baraza hilo limepanga kutumia michuano hiyo ili kuzipa timu za wanawake uzoefu zaidi wa kimashindano. Mulindwa amesema nchi zote za ukanda huu zina timu za wanawake hivyo wanataka kuandaa michuano hiyo ili kuwaweka pamoja na kukuza soka la kinamama. Mulindwa aliongeza kuwa tukio kama hilo ni muhimu kwani timu za taifa za wanawake huwa hazipati nafasi ya kucheza mechi nyingi za kimashindano kutokana na nchi nyingi kutokuwa na ligi ya soka wanawake.
No comments:
Post a Comment