Monday, August 11, 2014

KLOSE ATUNDIKA DARUGA KIMATAIFA.

MSHAMBULIAJI mkongwe wa kimataifa wa Ujerumani, Miroslav Klose ambaye ameweka rekodi akiwa na timu ya taifa ya nchi hiyo kwa kushinda michuano ya Kombe la Dunia mwezi uliopita amestaafu rasmi soka la kimataifa. Klose ambaye amefunga mabao mawili katika michuano hiyo iliyofanyika nchini Brazil ameweka rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika kwa kufikisha mabao 16. Klose amesema katika taarifa aliyotoa kuwa kushinda Kombe la Dunia nchini Brazil ilikuwa ni ndoto zake toka akiwa mdogo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 aliendelea kuwa ana furaha na anajivunia kutoa mchango mkubwa katika soka la Ujerumani kwa kipindi cha miaka 13 aliyoitumikia na anadhani huo ni wakati muafaka wa kufunga ukurasa huo. Klose ambaye ni mchezaji wa pili kucheza mechi nyingi zaidi kwa Ujerumani akiwa amecheza mechi 137 alianza kuitumikia nchi hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2001 na kuja kuwa mfungaji bora akifunga mabao 71 na kuipita rekodi ya miaka 40 ya Gerd Mueller aliyefunga mabao 68.

No comments:

Post a Comment