NGULI wa zamani wa soka wa Argentina, Diego Maradona amefumwa katika picha za video akimtandika kofi mwandishi wa habari. Tukio hilo limetokea wakati Maradona mwenye umri wa miaka 53 akitoka katika ukumbi aliompeleka mtoto wake wa kiume aitwaye Diego Fernando ili kuangalia michezo ya watoto katika Siku ya Watoto nchini humo. Maradona ambaye alishinda Kombe la Dunia akiwa mchezaji wa Argentina mwaka 1986 huku pia akiwa kocha wan chi hiyo kuanzia mwaka 2008 mpaka 2010 imekuwa kawaida yake kuzozana na waandishi habari. Mwaka 1994 alihukumiwa jela miaka miwili na miezi 10 kwa kufyatua risasi hewani kuwatawanya waandishi nyumbani kwake tukio ambalo watu wanne walijeruhiwa.
No comments:
Post a Comment