Friday, August 8, 2014

DONOVAN ATANGAZA KUSTAAFU MWISHONI MWA MSIMU WA MLS.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Marekani, Landon Donovan ametangaza kustaafu soka mwishoni mwa msimu wa Ligi Kuu ya Soka ya Marekani-MLS. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 32 ndiye mfungaji anayeoongoza kwa mabao katika timu yake ya taifa akiwa amefunga mabao 57 katika mechi 156. Donovan aliwahi kuitumikia Everton kwa kuichezea mechi 22 na kufunga mabao mawili alisajiliwa mara mbili kwa mkopo. Nyota huyo anayecheza timu ya Los Angeles Galaxy aliuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa baada ya kufikiri na kupata ushauri kutoka kwa watu wake wa karibu ameamua kuwa mwaka huu ndio utakakuwa wa mwisho kwake. Donovan ameshiriki katika fainali tatu za Kombe la Dunia akiwa na Marekani na pia amekuwa akiitwa katika kikosi cha wachezaji nyota wa MLS mara sita. Msimu wa MLS unatarajiwa kumalizika Octoba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment