KLABU ya Celtic imepata bahati ya kurejeshwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya timu ya Legia Warsaw kutimuliwa kwa kuchezesha mchezaji asiyeruhusiwa. Legia walishinda mzunguko wa tatu wa kufuzu kwa jumla ya mabao 6-1 lakini walimtumia mchezaji Bartosz bereszynski katika mechi yao ya mkondo wa pili wakati alikuwa akitumikia adhabu. Matokeo hayo yamepelekea Celtic kupewa ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wao wa mkondo wa pili hivyo kuwavusha hatua hiyo kwa bao la ugenini. Legia wamepewa siku tano za kukata rufani na wameliomba Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kuwapa sababu.
No comments:
Post a Comment