KOCHA Mfaransa Christian Gourcuff ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Algeria akichukua nafasi ya Vahid Halilhodzic. Shirikisho la Soka la Algeria lilithibitisha taarifa hiyo huku jukumu la kwanza alilopewa ni kuhakikisha nchi hiyo inafanikiwa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwakani na 2017 pamoja na michuano ya Kombe la Dunia 2018. Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Lorient mwenye umri wa miaka 59 pia atafundisha timu A iliyotengenezwa maalumu kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani. Kocha huyo atafanya kazi sambamba na nahodha wa zamani wa Alegria Yazid Mansouri ambaye alicheza chini yake katika timu ya Lorient na sasa ametajwa kama meneja mkuu wan chi hiyo. Halilhodzic ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yugoslavia alichukua mikoba ya kuinoa Algeria mwaka 2011 lakii alikataa kusaini mkataba mpya pamoja na kuivusha nchi hiyo katika hatua ya mtoano kwenye michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Brazil.
No comments:
Post a Comment