SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limemfungia mechi nane za kimataifa kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ugiriki Fernando Santos baada ya kutolewa nje mwishoni mwa mchezo wa Kombe la Dunia dhidi ya Costa Rica. Katika taarifa yake FIFA imedai kuwa Santos ambaye alitolewa nje mwishoni mwa dakika za nyongeza katika mchezo wa hatua ya mtoano Juni 29 mwaka huu, alikutwa na hatia ya kumzonga mwamuzi. Katika mchezo huo Costa Rica walishinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati na kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 aliacha kuifundisha Ugiriki baada ya michuano hiyo iliyomalizika nchini Brazil. Santos ambaye amekuwa akiinoa Ugiriki kwa miaka minne anatarajiw akuitumikia adhabu hiyo wakati atakapata nafasi ya kuinoa timu nyingine ya taifa. FIFA pia imesema kamati yake ya nidhamu imemfungia mechi sita za kimataifa mwalimu wa viungo wa timu ya taifa ya Italia Aldo Esposito baada ya kutolewa nje wakati nchi hiyo ilipotandikwa bao 1-0 na Uruguay katika hatua ya makundi.
No comments:
Post a Comment