Tuesday, August 5, 2014

EBOLA YALETA BALAA KATIKA SOKA SIERRA LEONE.

CHAMA cha Soka nchini Sierra Leone kimesimamisha shughuli zote za mchezo wa soka nchini humo kutokana na kuenea kwa kasi kwa ugonjwa wa Ebola. Uamuzi hu umefikiwa baada ya rais wa nchi hiyo, Ernest Bai Koroma wiki iliyopita kutangaza hali ya hatari kiafya katika nchi hiyo. Taarifa hiyo ya hali ya hatari inatarajiwa kudumu kwa miezi mitatu na kuhatarisha nafasi ya timu ya taifa ya nchi hiyo kushiriki hatua ya makundi ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Morocco. Sierra Leone walitarajiwa kucheza ugenini dhidi ya Ivory Coast Septemba 5 au 6 kabla ya kuikaribisha nyumbani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC Septemba 10 mwaka huu. Ofisa mmoja wa shirikisho hilo Abu Bakarr Kamara alikaririwa akidai kuwa wanamategemeo Ebola itaweza kudhibitiwa kabla ya mchezo wao dhidi ya RDC na kuweza kucheza katika uwanja wao nyumbani jijini Freetown lakini kama ikishindikana itabidi watafute uwanja huru kwa ajili ya mchezo huo. Sierra Leone ilifuka katika hatua ya makundi ya kufuzu baada ya Shelisheli kujitoa katika mchezo wao wa pili kwa ushauri wa wizara yao ya afya.

No comments:

Post a Comment