MWANAMAMA Corinne Diacre anayeinoa klabu ya Clermont Foot ya Ufaransa amepoteza mchezo wake wa kwanza akiwa kocha wa timu hiyo kwa kufungwa mabao 2-1 na timu ya Brest. Mechi hiyo ya Ligi Daraja la Pili nchini Ufaransa ilishuhudia kwa mara ya kwanza mwanamke akiisimamia timu ya wanaume kama kocha katika ligi ya Ulaya. Clermont ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Souleymane Sawadogo katika kipindi cha kwanza kabla ya wapinzania kufunga mabao mawili na kuibuka washindi katika kipindi cha pili. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Diacre amesema kufungwa siku zote sio jambo zuri lakini hana chaka kwamba timu yake itafanya vyema msimu huu. Kocha alisherekea miaka 40 ya kuzaliwa kwake jana na alipokea shahada la maua na busu katika shavu kutoka kwa kocha mwenzake wa timu pinzani ya Brest, Alex Dupont kabla ya kuanza kwa mchezo huo. Diacre alichukua mikoba ya kuinoa timu hiyo Juni mwaka huu akichukua nafasi ya mwanamke mwenzake Helena Costa ambaye alijiuzulu kabla ya kucheza mechi hata moja akiituhumu Clermont kwa kushindwa kumheshimu.
No comments:
Post a Comment