Tuesday, August 5, 2014

XAVI ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA.

KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Hispania, Xavi ametangaza kustaafu soka la kimataifa akiwa na umri wa miaka 34. Mchezaji huyo wa Barcelona ameiwakilisha nchi yake kwa rekodi ya mechi 133 na kuisaidia kushinda Kombe la Dunia mwaka 2010, na michuano ya Ulaya mwaka 2008 na 2012. Xavi aliwaambia waandishi wa habari kuwa anajivunia kwa miaka yote aliyoiwakilisha nchi yake kwani wamefanya mengi mazuri. Nyota huyo aliongeza kuwa kwasasa hana miaka 20 tena lakini bado ana morali kama mtoto mdogo. Xavi pia alikuwa mmoja ya wachezaji wa Hispania walioshindwa kuvuka hatua ya mzunguko wa kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Brazil mwaka huu.

No comments:

Post a Comment