NYOTA wa klabu ya Barcelona Neymar na Lionel Messi wamerejea mazoezini leo baada ya likizo ndefu ya Kombe la Dunia wakiwa sambamba na Javier Mascherano na Dani Alves. Hatua ya fainali iliyofikiwa na Argentina katika michuano hiyo imesaidiwa kwa kiasi kikubwa na Messi na Mascherano wakati Alves alikuwa sehemu ya kikosi cha Brazil kilichimaliza katika nafasi ya nne na sasa kocha mpya Luis Enrique anaweza kuwajumuisha wachezaji hao katika maandalizi ya msimu mpya. Neymar ambaye aliumia mgongo katika mchezo war obo fainali dhidi ya Colombia yeye amerejea lakini hataweza kujiunga na wenzake wakati akiendelea kupona badala yake atakuwa akifanya mazoezi peke yake. Mechi za kirafiki za Barcelona walizocheza mpaka sasa zimekuwa za kusuasua ambapo wameambulia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Recreativo Huelva na sare ya bao 1-1 baada ya wiki tatu za mazoezi. Hata hivyo bado wanakabiliwa na mechi zingine za kujipima nguvu dhidi ya Napoli, HJK na Leon kabla ya kucheza mechi yao ya ufunguzi wa La Liga dhidi ya Elche Agosti 24 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment