Wednesday, August 13, 2014

HATIMAYE BOSI WA ZAMANI WA MICROSFT AINUNUA LOS ANGELES CLIPPERS.


OFISA mkuu wa zamani wa kampuni ya Microsoft, Steve Ballmer ameinunua klabu ya mpira wa kikapu ya Los Angeles Clippers kwa dola bilioni 2 baada ya mahakama kuruhusu kuuzwa kwa timu hiyo. Jaji wa mahakama jijini Los Angeles alithibitisha kuwa Shelly Sterling anaweza kuiuza timu hiyo pamoja na hatua hiyo kupingwa na mumewe Donald Sterling. Sterling ambaye amekuwa mmiliki wa timu hiyo toka mwaka 1981 alifungiwa maisha kujishughulisha na mambo ya michezo baada ya kurekodiwa akitoa kauli za kibaguzi. Mauzo ya dola bilioni 2 ndio makubwa zaidi kuwahi kulipwa kwa ajili ya timu inayoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani maarufu kama NBA.

No comments:

Post a Comment