MAHAKAMA ya Kimataifa ya Usuluhishi ya Michezo-CAS imedai kuwa hatma ya rufani ya mshambuliaji nyta wa kimataifa wa Uruguay Luis Suarez kupinga adhabu aliyopewa kwa kumng’ata Giorgio Chiellini itajulikana kesho. Suarez alifungiwa mechi tisa za kimataifa na kutojishughulisha na mambo yoyote yahusuyo soka kwa miezi minne baada ya kufanya tukio hilo katika mchezo wao wa hatua ya makundi Italia kwenye michuano ya Kombe la Dunia. Baada ya kushindwa rufani yake kwa Shirikisho la Soka Duniani-FIF, mshambuliaji huyo wa Barcelona alipeleka kesi hiyo CAS ambayo ilisikiliza shauri hilo Ijumaa iliyopita. Katika taarifa yake CAS ilithibitisha kuwa itatoa uamuzi wake kuhusiana na rufani hiyo kesho.
No comments:
Post a Comment