SHIRIKISHO la Soka la Libya limetaka mchezo wa mtoano dhidi ya Congo Brazzaville ili kujua atayechukua nafasi ya Rwanda katika makundi ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kufuatia kundolewa kwa nchi hiyo kwa kumtumia mchezaji mwenye majina mawili tofauti. Maofisa wa Libya walituma malalamiko yao Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF dhidi ya Rwanda baada ya kufungwa mabao 3-0 katika mzunguko wa kwanza uliochezwa Mei mwaka huu lakini shirikisho hilo likadai kuwa vielelezo vilivyowasilishwa na nchi hiyo havikutosheleza. Mshambuliaji wa Rwanda aliyeleta Dady Birori alifunga mabao yote matatu katika mchezo wa marudiano dhidi ya Libya na kuitoa nchi hiyo baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa kwanza. Birori pia alichezeshwa wakati Rwanda wakifuzu kucheza makundi dhidi ya Congo Brazzaville kabla ya maofisa wake kutuma malalamiko yao CAF ya kumlalamikia mchezaji huyo anayetuhumiwa kuwa na pasi mbili za kusafiria zenye majina tofauti. CAF kwasasa wainyang’anya nafasi Rwanda na kuipa Congo lakini Libya nao pia walikuwa wahanga wa mchezaji huyo kutumika katika mechi yao ndio maana wameamua kutaka mchezo wa mtoano ili kuamua atayechukua nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment