KLABU ya Real Madrid, inatarajiwa kumfanyia uchunguzi mshambuliaji Cristiano Ronaldo baada ya kuumia mgongo katika mchezo wa Super Cup dhidi ya Atletico Madrid ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1. Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 alibadilishwa katika muda wa mapumziko kwenye mchezo huo wa jana na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mpya aliyesajiliwa kiangazi hiki James Rodriquez ambaye aliifungia timu hiyo. Meneja wa Madrid Carlo Ancelotti amesema Ronaldo alikuwa akicheza kwa maumivu ambapo wanatarajia kumfanyia vipimo ili kugundua tatizo limalomkabili lakini hadhani kama litakuwa tatizo kubwa sana. Ronaldo alipata maumivu ya goti ya msuli wakati michuano ya Kombe la Dunia ambapo Ureno ilishindwa kuvuka hatua ya makundi lakini alirejea na kufunga mabao mawili katika mchezo wa Super Cup ya Ulaya dhidi ya Sevilla uliochezwa katika Uwanja wa Cardiff wiki iliyopita. Nyota huyo mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or ameifungia mabao 51 Madrid msimu uliopita yakiwemo 17 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuisaidia timu hiyo kunyakuwa taji.
No comments:
Post a Comment