Wednesday, August 20, 2014

FIFA YAIKOMALIA BARCELONA KUSAJILI, SASA WAAMUA KUKIMBILIA CAS.

KLABU ya Barcelona haitaruhusiwa kusajili mchezaji yeyote mpaka Januari mwaka 2016 mara dirisha la sasa la usajili litakapofungwa baada ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kutupilia mbali rufani yao kupinga adhabu ya kufungiwa. Barcelona walipewa adhabu ya kufungiwa miezi 14 baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja sheria za usajili wa wachezaji wa kimataifa walio chini ya umri wa miaka 18. Adhabu hiyo ilisimamishwa kutokana na rufani waliyokata na kuwaruhusu kumsajili Luis Suarez na adhabu hiyo sasa itaanza kufanya kazi katika dirisha lijalo la usajili mapema Januari mwakani. Hiyo inamaanisha kuwa usajili wa kiangazi hiki hautaathirika kama klabu hiyo itataka kusajili wachezaji zaidi kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Agosti 31 mwaka huu. Hata hivyo, taarifa zilitumwa katika mtandao wa klabu hiyo zimedai kuwa watakata rufani nyingine katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS kuendelea kupinga adhabu hiyo.

No comments:

Post a Comment