Wednesday, August 20, 2014

SWANSEA YANASA BEKI LA ARGENTINA.

KLABU ya Swansea City imefanikiwa kumsajili beki wa kimataifa wa Argentina, Federico Fernandez kutoka Napoli kwa ada ambayo haikuwekwa wazi. Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 25 ameichezea nchi yake mechi 25, alicheza mechi nne katika michuano ya Kombe la Dunia ambayo Argentina walitinga fainali. Fernandez alitia saini mkataba wa miaka minne baada ya kufaulu vipimo vya afya jana. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo, ilithibitisha kumsajili mchezaji huyo huku akitarajiwa kucheza katika mchezo wa Ligi Kuu Jumamosi ambapo Swansea watakuwa wenyeji wa Burnley baada ya kuitandika Manchester United wiki iliyopita. Fernandez alikuwa sehemu ya kikosi cha Napoli kilichonyakuwa Kombe la Italia msimu uliopita na kucheza katika michuano yote ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League.

No comments:

Post a Comment