Friday, August 22, 2014

HOWARD KUPUMZIKA MWAKA MMOJA KUITUMIKIA MAREKANI.

GOLIKIPA wa klabu ya Everton, Tim Howard ametangaza kupumzika kwa mwaka mmoja kuitumikia timu ya taifa ya Marekani ili aweze kupata muda wa kukaa na familia yake. Golikipa huyo mwenye umri wa miaka 35 ambaye amecheza mechi 104 za kimataifa amesema atapumzika mpaka Septemba 2015 hatua ambayo itamfanya kukosa michuano ya Kombe la Dhahabu inayoandaliwa na Concacaf. Akihojiwa Howard amesema kutenga muda kwa ajili ya familia yake ni jambo la muhimu sana kwa wakati huu na atarejea mwakani ili kugombea tena nafasi yake. Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi, Jurgen Klinsmann aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa amefanya mazungumzo ya kina na Howard na anaheshimu uamuzi wake. Klinsmann ambaye aliiongoza Marekani kuvuka hatua ya mtoano katika michuano ya Kombe la Dunia aliongeza kuwa hatua hiyo ya Howard itatoa nafasi kwa makipa wengine akiwemo Brad Guzan wa Aston Villa na Nick Rimando wa Real Salt lake kugombea nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment