LIGI KUU nchini Uingereza ambayo imeanza jumamosi iliyopita itaendelea tena leo ambapo Burnley waliopanda daraja msimu huu watawakaribisha Chelsea kwenye Uwanja wa Turf Moor. Burnley huenda wakawatumia wachezaji wake mahiri akiwemo Lukas Yukiviz ambaye amesajiliwa msimu huu akiungana na Danny Ings kuunda safu bora ya ushambuliaji kama ambavyo wamejidhihirisha ubora wao katika michezo ya majaribio kabla ya ligi. Chelsea wao huenda kocha Jose Mourinho akawaanzisha wachezaji wake wapya Cesc Fabregas, Diego Costa na Filipe Luis na bila shaka golikipa Thibaut Courtois. Chelsea pia wanaweza kutumia nafasi hiyo kumjaribu mgongwe Didier Drogba aliyekuwa majeruhi, huku wachezaji wengine kadhaa wakielezwa kuwa na hofu ya majeraha.
No comments:
Post a Comment