Monday, August 18, 2014

ATLETICO, REAL MADRID KUKWAANA KATIKA SUPER CUP.

MABINGWA wa La Liga Atletico Madrid wana nafasi ya mapema kulipa kisasi cha kufungwa na mahasimu wao Real Madrid katika mchezo wa nusu fainali uliofanyika Mei mwaka huu wakati watakapokutana katika mchezo wa mkondo wa kwanza Super Cup hapo kesho. Pamoja na kuwa na msimu mzuri uliopita, Atletico bado walipata matatizo ya kuondokewa na nyota wake kadhaa akiwemo Filipe Luis na Diego Costa waliojiunga na Chelsea na Thibaut Courtois naye alirejea Stamford Bridge baada ya miaka mitatu aliyokuwa akicheza kwa mkopo. Kitita kilichopatikana kwa mauzo ya Costa na Filipe hata hivyo kilisaidia kuongeza nguvu baada ya kuwasajili Mario Mandzukic kutoka Bayern Munich na nyota wa kimataifa wa Mexico Raul Jimenez aliyetokea Club America. Super Cup ni taji ambalo meneja wa Atletico Diego Simeone hatafanikiwa kulipata katika kipindi cha miaka mitatu aliyoinoa timu hiyo baada ya kushindwa kwa bao la ugenini mbele ya Barcelona msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment