Monday, August 18, 2014

DZEKO MBIONI KUSAINI MKATABA MPYA CITY.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Manchester City Edin Dzeko ambaye aliisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu jana, anatarajiwa kusaini mkataba mpya ambao utamuweka hapo kwa kipindi cha mitano mingine. Nyota huyo wa kimataifa wa Bosnia kwasasa amebakisha miezi 10 pekee katika mkataba wake na nia ya meneja Manuel Pellegrini kumbakisha mchezaji huyo iliongezeka baada ya kuonyesha kiwango cha juu katika mchezo dhidi ya Newcastle. Pellegrini amesema Dzeko alimaliza msimu uliopita akiwa amecheza vizuri na kuwaunganisha vyema wenzake ndio maana ameamua kuendelea kuwa naye kwani atakuwa msaada mkubwa kwa siku zijazo. City inakabiliwa na mchezo mgumu wa ligi unaofuata dhidi ya Liverpool utakaochezwa mwishoni mwa wiki hii.

No comments:

Post a Comment