MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anafikiria kumrejesha beki Per Martesacker mapema kwa ajili ya mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Besiktas, kutokana na kuandamwa na majeruhi. Martesacker na wachezaji wenzake wa Ujerumani Mesut Ozil na Lukas Podolski walipewa likizo zaidi na Wenger baada ya kushinda taji la Kombe la Dunia nchini Brazil mwezi uliopita. Hata hivyo kutokana na kuumia kwa mabeki Laurent Koscielny na Kieran Gibbs katika mchezo wa Jumamosi iliyopita dhidi ya Crystal Palace inaaminisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Wenger kumtumia Martesacker katika mchezo wao wa kesho. Wenger amesema ataona kama Koscielny atakuwa fiti kwa wakati lakini kama hatakuwa fiti itabidi amrejeshe Matersacker katika kikosi chake kutokaa na umuhimu wa mchezo wenyewe. Arsenal imefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika misimu 17 mfululizo.
No comments:
Post a Comment