Monday, August 18, 2014

BA AMPONDA MOURINHO KWA KUCHAGUA MAJINA.

MSHAMBULIAJI zamani wa Chelsea, Demba Ba amemshambulia Jose Mourinho akidai kuwa kocha huyo amekuwa akijali zaidi heshima kuliko mipango. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal alijiunga na klabu ya Besiktas kiangazi hiki baada ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza Stamford Bridge, huku ujio wa Diego Costa ikififisha matumaini yake kabisa. Ba ambaye amefunga mabao muhimu wakati akiwa Chelsea amedai kuwa hakupewa nafasi ya kutosha ili kuonyesha uwezo wake mbele ya Mourinho kwa Fernando Torres kupewa nafasi zaidi yake. Nyota amedai kuwa muda mwingine kunapokuwa nyota wengi katika klabu jina ndio huwa linambeba mtu na sio mipango na hilo anadhani ndio lililotokea kwake. Hata hivyo Ba amesema alifuahi kujiunga na Chelsea akitokea Newcastle na kupata mafanikio aliyopata ikiwemo kujitengenezea marafiki wengi.

No comments:

Post a Comment