Monday, August 18, 2014

PELLEGRINI KUACHA WANNE CITY.

MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini amebainisha kuwa anapanga kuwaacha nyota wake Matija Nastasic, Micah Richards, Scott Sinclair na John Guidetti katika kipindi hiki cha kiangazi. Pellegrini amesema Matija anahitaji muda zaidi kwa kucheza lakini tayari wanao wachezaji wengine wanne wanaocheza nafasi yake ya beki wa kati akiwemo Martin Demichelis, Vicent Kompany, Eliaquim Mangala na Dedryck Boyata. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa katika siku chache zijazo wataona jinsi gani itakavyokuwa kwa Matija, ni mchezaji muhimu kwao lakini anapenda apate muda zaidi wa kucheza ndio maana anaweza kumuachia kama ikija ofa nzuri. Richards nay eye anataka kuondoka kwa ajili ya kuhitaji muda zaidi wa kucheza huku vilabu vya Liverpool, Tottenhham Hotspurs, Newcastle United na Everton zote zikionyesha kumhitaji.

No comments:

Post a Comment