Monday, August 18, 2014

UNITED YAMTENGEA DI MARIA PAUNDI MILIONI 50.

KUFUATIA kuanza vibaya msimu mpya wa Ligi Kuu, Manchester United wanaripotiwa kujiandaa kutumia kiasi kikubwa cha fedha katika dirisha hilo la usajili. United kwasasa inajipanga kutenga kitita cha paundi milioni 50 kwa ajili ya winga wa Real Madrid angel di Maria ambaye anaonekana kukosa nafasi katika timu hiyo toka ujio wa James Rodriguez aliyetokea Monaco. Kwa mujibu wa mtandao wa Daily mail United wametenga jumla ya paundi milioni 100ikiwemo mkataba wa miaka mitano kwa nyota huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 26. Klabu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa ndio wamekuwa wakiongoza mbio za kumuwania Di Maria lakini walijitoa kutokana na kushindwa gharama zilizowekwa kwa ajili ya usajili wake.

No comments:

Post a Comment