MENEJA mpya wa klabu ya Manchester United, Luis van Gaal anatarajia kuwahabarisha wachezaji asiowahitaji uso kwa uso baada ya kumalizika kwa ziara yao ya Marekani ili kuwapa muda wa kutafuta vilabu vingine. Anderson, Nani, Javier Hernandez, Shinji Kagawa na Marouane Fellaini ni miongoni mwa wachezaji wenye majina makubwa ambao wako katika hatari ya kuondoka kabla ya dirisha la usajili majira ya kiangazi halijafungwa. Akihojiwa Van Gaal amesema atatoa maamuzi baada ya ziara hiyo kwasababu amewapa nafasi wachezaji wote kucheza na sasa anawafahamu kuliko ilipokuwa hapo mwanzo. Kocha huyo amesema amejaribu kumsoma kila mchezaji na anajua wapi anaowahitaji na wapi asiowahitaji hivyo atatoa uamuzi wa mwisho baada ya ziara hiyo ili kuwapa nafasi wanaoondoka kutafuta vilabu vingine vya kwenda. United inatarajiwa kuchuana na Liverpool katika mchezo wa fainali ya kirafiki ya michuano ya kimataifa itakayofanyika katika Uwanja wa Sun Life jijini Miami baadae leo.
No comments:
Post a Comment