KLABU ya Real Madrid imefanikiwa kumsajili golikipa wa kimataifa wa Costa Rica, Keylor Navas kwa mkataba wa miaka sita. Navas alikuwa nyota katika michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika nchini Brazil mwezi uliopita kwa kuisaidia nchi yake kutinga hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 anatua Santiago Bernabeu akitokea klabu ya Levante nayo ikiwa inashiriki La Liga. Inaaminika kuwa Madrid ambayo ni mabingwa wa Ulaya wametoa kitita cha paundi milioni 7.9 kwa ajili ya saini ya kipa huyo. Navas anatarajiwa kutambulishwa rasmi mbele ya mashabiki katika Uwanja wa Santiago Bernabeu kesho baada ya kufanyiwa vipimo vya afya. Golikipa huyo anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Madrid kiangazi hiki baada ya kuwasajili Toni Kroos kutoka klabu ya Bayern Munich na James Rodriguez kutoka Monaco.
No comments:
Post a Comment