Monday, August 4, 2014

VERMAELEN AKOMAA KUONDOKA ARSENAL.

BEKI mahiri wa klabu ya Arsenal, Thomas Vermaelen ameonyesha kutokuwa tayari kusaini mkataba mpta na klabu hiyo hivyo kumuweka katika nafasi ya kuondoka kiangazi hiki. Mkataba wa nahodha huyo wa Arsenal unatarajiwa kumalizika mwakani na klabu inaonyesha iko tayari kumpatia mkataba mwingine lakini mwenye hataki kuanza mazungumzo ya mkataba mpya. Kama Arsenal watashindwa kumuuza beki huyo katika kipindi cha usajili wa kiangazi, inamaanisha kuwa anaweza kufikia makubaliano ya mkataba a klabu nyingine kuanzia Januari. Arsenal wanaonekana kutotaka kumuuza nahodha wao huyo kiangazi hiki, lakini pia wanataka kuepuka uwezekano wa kukosa chochote kutoka kwake mwakani. Klabu za Barcelona, Manchester United na Napoli zote zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili beki huyo.

No comments:

Post a Comment