Monday, August 4, 2014

OBI MIKEL KUNG'ANG'ANIA CHELSEA.

KIUNGO wa kimataifa wa Nigeria, John Obi Mikael amesisitiza kuwa atabakia na kupambania nafasi yake katika kikosi cha timu ya Chelsea. Mikel alipoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza cha Chelsea kufuatia ujio wa kiungo wa Serbia Nemanja Matic Januari mwaka huu. Kulikuwa na tetesi kuwa kiungo huyo angeondoka Stamford Bridge katika kipindi hiki cha usajili wa kiangazi lakini Mikel mwenye amekanusha vikali tetesi hizo. Akihojiwa Mikel amesema amekuwa na timu hiyo kwa miaka mingi kwani amekuja hapo akiwa na umri wa miaka 18 na sasa ameshafikisha 27. Nyota huyo ameendelea kudai kuwa kumekuwa na wakati na mzuri na pia wakati mbaya akiwa na wakongwe kama John Terry na Petr Cech na mara zote mambo yanapokwenda vibaya wamekuwa wakiungana pamoja kama timu na kujikwamua. Mikel amesema amekuwa akifanya mazoezi kwa nguvu kuhakikisha anarejesha makali yake ili aweze kupigania nafasi yake pindi msimu mpya wa ligi utakapoanza baadae mwezi huu.

No comments:

Post a Comment