Wednesday, August 13, 2014

VIEIRA AISHANGAA RAIS MBAGUZI WA RANGI KUCHANGULIWA KUONGOZA SOKA ITALIA.

KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, Patrick Vieira amedai kutoamini kama Italia imemchagua Carlo Tavecchio kuwa rais mpya wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo baada ya kuingia katika mzozo wa kibaguzi. Tavecchio mwenye umri wa miaka 71 ambaye wakati akigombea nafasi hiyo alitoa kauli za kibaguzi kuhusiana na mchezaji wa Kiafrika Opti Poba kula ndizi, alishinda kwa asilimia 63.63 ya kura zote zilizopigwa Jumatatu iliyopita dhidi ya mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Italia na AC Milan Demetrio Albertini. Vieira ambaye enzi zake amewahi kuichezea Juventus na Inter Milan amesema anapata wakati mgumu kuamini kama Tavecchio ameteuliwa kuwa rais wa shirikisho hilo baada ya kauli aliyoitoa. Vieira amesema kwa upande wake hiyo inamuonyesha jinsi gani mamlaka ya soka nchini Italia ilivyokuwa mbali katika suala la kupambana na ubaguzi wa rangi ambapo asilimia 63.63 ya waliompigia wameonyesha jinsi walivyokuwa hawako tayari kupambana na suala hilo. Nyota huyo ambaye kwasasa ni mkurugenzi wa kukuza vipaji katika klabu ya Manchester aliendelea kudai kuwa amecheza soka Italia kwa miaka kadhaa hivyo anajua suala kwasababu alishakuwa mhanga wa matukio ya kibaguzi.

No comments:

Post a Comment