KLABU ya AC Milan imeitaka Al Ahly kulipa kiasi cha euro milioni 1.5 ili kucheza nao mchezao wa kirafiki jijini Cairo Octoba mwaka huu. Bodi ya klabu hiyo imeamua kusheherekea baada ya kuwa klabu ya yenye mafanikio zaidi kwa mataji ya kimataifa waliyoshinda wakizipita klabu za Boca Juniors ya Argentina na wakongwe wa Italia Milan baada ya kushinda taji la Kombe la Super Cup Februari mwaka huu. Klabu hiyo imetuma maombi kwa vilabu mbalimbali kuomba mchezo huo wa kirafiki na Milan ni mojawapo sambamba na Boca Juniors. Chanzo kimoja kutoka ndani ya klabu hiyo kilibainisha kuwa Milan wametaka kiasi hicho cha pesa ili waweze kwenda Cairo kwa ajili ya mchezo huo lakini maofisa wake wanadhani kiasi hicho ni kikubwa sana na hawadhani kama wataweza kukimudu. Chanzo hicho hicho kiliendelea kudai kuwa bodi ya klabu hiyo ina matumaini ya kuwashawishi wadhamini ili kuona kama wanaweza kusaidia sehemu ya gharama kwa ajili ya mchezo huo na Milan.
No comments:
Post a Comment