Friday, September 19, 2014

PARDEW AWAANGUKIA MASHABIKI WA NEWCASTLE KUPUNGUZA JAZBA.

MENEJA wa klabu ya Newcastle United, Alan Pardew amewatuhumu mashabiki kuwa na jazba baada ya kikosi chake kuanza vibaya msimu huu wa Ligi Kuu. Pardew pia amesema kuwa mashabiki wamekuwa wakiwaathiri wachezaji kwa kuwakosoa sana. Meneja huyo aliendelea kudai hakutaka kuhakikishiwa kibarua chake katika mkutano na mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley kufuatia kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Southampton ambacho kimewaacha wakiburuza mkia katika msimo wa ligi. Newcastle wamembulia alama mbili pekee katika mechi nne walizocheza na keshop wanakabiliwa na mchezo dhidi ua Hull City huku kukiwa na tetesi za mustabali wa Pardew. Pardew amesema ana matumaini ya kubadilisha mambo lakini mazingira kwa wachezaji kesho anatarajiwa kuwa magumu zaidi kuliko ilivyokuwa kabla kwani inaweza kufikia hatyua mpaka wachezaji kushindwa kucheza kwa kiwango chao.

No comments:

Post a Comment